MATUMIZI YA FASIHI SIMULIZI KATIKA KAMPENI ZA UCHAGUZI TANZANIA

How to Cite

MATUMIZI YA FASIHI SIMULIZI KATIKA KAMPENI ZA UCHAGUZI TANZANIA: TATHMINI YA DHIMA YA NYIMBO. (2024). JARIDA LA CHAUKIDU. https://doi.org/10.0255/vyxkp073

Share

Abstract

Fasihi simulizi kama chombo cha kazi cha jamii haiwezi kujitenga na jamii katika
shughuli zake kama vile za kiuchumi, kiutamaduni, kijamii, na kisiasa. Makala
haya yanaeleza matumizi ya fasihi simulizi katika kampeni za siasa nchini
Tanzania kwa kutumia kipengele cha nyimbo. Makala yanaeleza kuwa nyimbo ni
nyenzo mojawapo inayotumika katika michakato ya kisiasa ikiwa ni pamoja na
mikutano ya kampeni za uchaguzi. Data za makala haya zinazotokana na nyimbo
za kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 zilizotumika kueleza falsafa,
sera, dira, na matarajio ya wanasiasa katika ugombea wao wa nafasi za uongozi wa
kisiasa. Kwa kutumia Nadharia ya Uhalisia wa Urasimi, makala haya yanaonesha
kuwa nyimbo za kampeni za uchaguzi zinatumika kueleza ukweli wa mambo bila
kutia chuku. Nyimbo hizi ziznaeleza mambo dhahiri ya kila siku na yanayoweza
kuthibitika. Makala haya yanaeleza kuwa mbinu ya matumizi ya nyimbo katika
kampeni za kisiasa za Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015, na bila shaka katika
kampeni zilizotangulia na zile zitakazokuja baadaye, ilitumika kipragmatiki kwa
minajili ya kufikia matarajio ya kisiasa ya makundi ya wanasiasa na vyama vya
siasa kwa ujumla. Kwa upande mmoja, mbinu hiyo ilikuwa na lengo la kutengeneza
hadhara za wapiga kura na kuiweka tayari kwa ajili ya kusikiliza kampeni na
hatimaye baadaye kupiga kura. Hali kadhalika, ilikuwa na azma ya kueleza na
kusifu sera na falsafa za wagombea na vyama vyao vya siasa. Vilevile, ilikuwa ni
mbinu ya kupinga sera na falsafa ya wagombea na vyama vingine. Katika makala
haya, inaelezwa kuwa, pamoja na malengo hayo, lengo kuu kupita yote la kutumia
mbinu ya nyimbo, kama kipengele cha fasihi simulizi, ilikuwa hatimaye kupata
ushindi katika uchaguzi wenyewe.

Creative Commons License

This work is licensed under a Creative Commons Attribution 4.0 International License.

Copyright (c) 2024 JARIDA LA CHAUKIDU

Downloads

Download data is not yet available.