Abstract
Makala haya yanaangazia matumizi ya lugha katika riwaya inayosadikiwa kuwa
ya kwanza ya Kiswahili ya Uhuru wa Watumwa (1934) iliyoandikwa na James
Mbotela na riwaya ya kwanza ya Kiswahili ya majaribio ya Nagona (1990) ya
Euphrase Kezilahabi, iliyoandikwa takribani miaka hamsini baadaye. Makala
yanajadili matumizi ya lugha ya Kiswahili kwa kuangalia tofauti za matumizi yake
katika riwaya hizo mbili za Kiswahili, vikiwamo vipengele kama vile vya uteuzi wa
msamiati, lugha ya usimulizi, lugha ya majigambo, lugha ya ucheshi na kadhalika.
Pia, makala yanajadili jinsi ambavyo riwaya hubadilika ikiendana na mabadiliko
yanayoendelea kutokea katika jamii.
This work is licensed under a Creative Commons Attribution 4.0 International License.
Copyright (c) 2024 JARIDA LA CHAUKIDU