MABADILIKO YA KIJAMII NA USAWIRI WA MWANAMKE
Inahitaji Usajili PDF

Jinsi ya Kunukuu

MABADILIKO YA KIJAMII NA USAWIRI WA MWANAMKE: UCHAMBUZI WA WIMBO WA TAARABU WA ISHA RAMADHANI. (2024). JARIDA LA CHAUKIDU. https://doi.org/10.0255/87dpsp27

##plugins.generic.shariff.share##

Muhtasari

Kihistoria mwanamke katika jamii amekuwa ni chombo kilicho katika mabadiliko
ya aina mbalimbali katika vipindi tofautitofauti. Mabadiliko hayo, hujitokeza
takriban karne mpaka karne kulingana na mifumo ya jamii husika. Kwa mfano,
yamejitokeza katika mfumo wa kijamaa, kimwinyi, kibepari kwa kutaja baadhi tu.
Katika kila mfumo tunaona jinsi mwanamke anavyosawiriwa kupitia kazi
mbalimbali za fasihi ya Kiswahili kuanzia kipindi cha utawala wa Waarabu wa
Omani wakati wa ukoloni katika Afrika Mashariki mpaka kipindi tulichopo sasa.
Wanawake katika jamii za Kiafrika, wanakumbana na changamoto za aina
mbalimbali katika jamii zinazotawaliwa na wanaume. Hali hii imesababisha
kuwapo kwa harakati za kumkomboa mwanamke dhidi ya mfumo kandamizi
kutoka kwa mwanamume. Je, ukombozi huo umepatikana au la? Makala haya,
yana lengo la kufafanua usawiri wa mwanamke katika karne hii ya ishirini na moja
sambamba na kubainisha mambo yaliyosababisha kuwapo kwa mabadiliko hayo
katika usawiri wa mwanamke. Mifano itatoka katika wimbo ulioimbwa na Isha
Ramadhani unaoitwa ‘Mwanamke Mpango Mzima’. Pia, makala haya,
yanachambua wimbo uliotungwa na kuimbwa na mwanamke ili kuweza kubaini
mtazamo wa mwanamke mwenyewe juu ya wanawake wenzake wa jamii za Afrika
Mashariki kwa ujumla.

Inahitaji Usajili PDF
Leseni ya Creative Commons

Kazi hii imewekwa chini ya Leseni ya Creative Commons Kutambulisha 4.0 Kimataifa.

Hakimiliki (c) 2024 JARIDA LA CHAUKIDU

Upakuaji

Data ya upakuaji bado haijapatikana.