DHIMA NA CHANGAMOTO ZA MATUMIZI YA TAFSIRI KATIKA UFUNDISHAJI WA KISWAHILI NCHINI UGANDA
Inahitaji Usajili PDF

Jinsi ya Kunukuu

DHIMA NA CHANGAMOTO ZA MATUMIZI YA TAFSIRI KATIKA UFUNDISHAJI WA KISWAHILI NCHINI UGANDA. (2024). JARIDA LA CHAUKIDU. https://doi.org/10.0255/bmqbm254

##plugins.generic.shariff.share##

Muhtasari

Ufundishaji wa lugha ya kigeni au lugha ya pili kwa wanafunzi wenye umilisi wa
lugha na desturi zao si jambo rahisi. Wakati mwingine, walimu hutumia tafsiri ili
wanafunzi waweze kuelewa vipengele vya lugha ya kigeni inayofundishwa. Makala
haya yanaangazia matumizi ya mbinu ya tafsiri katika shule za sekondari jijini
Kampala nchini Uganda. Lengo la makala haya ni kujadili iwapo tafsiri inaweza
kutambuliwa kama stadi ya tano katika ufundishaji wa Kiswahili kwa wageni.
Utafiti huu umechochewa na mkanganyiko uliopo kuhusu nafasi ya tafsiri katika
ufundishaji wa lugha. Ingawa tafsiri hutumiwa katika ufundishaji wa Kiswahili
kama lugha ya kigeni, mbinu hii haibainishwi kama mbinu mojawapo ya ufundishaji
kwenye mitaala. Data za utafiti ni za uwandani na maktabani. Data za uwandani
zilikusanywa kwa njia ya ushuhudiaji, hojaji na uchambuzi wa nyaraka. Matokeo
yanaonesha kwamba tafsiri ni mbinu inayotumiwa kwa upana katika ufundishaji
wa Kiswahili nchini Uganda. Halikadhalika, makala haya yamebainisha kuwa
Kiswahili ni lugha ya kigeni nchini Uganda, hali inayowafanya walimu kutegemea
tafsiri baina ya Kiswahili na Kiingereza. Kwa kuhitimisha, makala haya
yanashadidia kwamba hata kama tafsiri ina changamoto zake katika ufundishaji
wa lugha za kigeni, haiwezi kukwepeka katika ufundishaji wa Kiswahili katika
mazingira ambamo lugha hii haitumiwi katika mawasiliano ya kila siku.

Inahitaji Usajili PDF
Leseni ya Creative Commons

Kazi hii imewekwa chini ya Leseni ya Creative Commons Kutambulisha 4.0 Kimataifa.

Hakimiliki (c) 2024 JARIDA LA CHAUKIDU

Upakuaji

Data ya upakuaji bado haijapatikana.