‘HURUMA ILIGEUKA MVUKE’: UCHAMBUZI WA SITIARI ZA HISIA KATIKA KAZI ZA FASIHI YA KISWAHILI
Inahitaji Usajili PDF

Jinsi ya Kunukuu

‘HURUMA ILIGEUKA MVUKE’: UCHAMBUZI WA SITIARI ZA HISIA KATIKA KAZI ZA FASIHI YA KISWAHILI. (2024). JARIDA LA CHAUKIDU. https://doi.org/10.0255/kc2kgw62

##plugins.generic.shariff.share##

Muhtasari

Katika lugha ya kawaida na lugha ya kifasihi tunatumia sitiari nyingi zinazotusaidia
kuelezea yale mambo dhahania ya maisha, kama vile hisia, ambazo ni ngumu
kufahamisha na kuelezeka vinginevyo. Katika fasihi ya Kiswahili tunapata picha
nyingi za sitiari zinazoelezea mambo ya kihisia. Suala la kinachowasilishwa na
sitiari na tuzichukulie vipi, ni mjadala unaoendelea na ambao unalinganisha asili ya
sitiari na matumizi yake ya kimtindo katika fasihi. Katika muktadha wa fasihi,
tunajiuliza swali hili: je, ni nini kinachotofautisha misemo ya sitiari za kifasihi na
zile nahau zinazotumika katika lugha ya kawaida? Lengo la utafiti huu ni
kuchambua misemo ya sitiari inayotumika katika lugha ya Kiswahili, ili kutambua
zile sifa za lugha za kipekee ambazo zinaunda ‘creative blends’ za lugha ya kifasihi.
Makala hii inazingatia uchambuzi wa hisia katika lugha ya Kiswahili, hasa kwa
kuangalia kwa undani mifano ya sitiari zinazolenga dhana ya ‘joto’. Katika
uchambuzi unaofuata, nitaonesha mifano kadhaa kutoka kongoo lililoundwa hasa
na nathari za kisasa za Kiswahili.

Inahitaji Usajili PDF
Leseni ya Creative Commons

Kazi hii imewekwa chini ya Leseni ya Creative Commons Kutambulisha 4.0 Kimataifa.

Hakimiliki (c) 2024 JARIDA LA CHAUKIDU

Upakuaji

Data ya upakuaji bado haijapatikana.