LUGHA YA KIDIJITALI KAMA LUGHA YA KIMAZUNGUMZOANDISHI: MFANO WA MAWASILIANO YA FACEBOOK
issue
Inahitaji Usajili PDF

Jinsi ya Kunukuu

LUGHA YA KIDIJITALI KAMA LUGHA YA KIMAZUNGUMZOANDISHI: MFANO WA MAWASILIANO YA FACEBOOK. (2024). JARIDA LA CHAUKIDU. https://doi.org/10.0255/whaanp96

##plugins.generic.shariff.share##

Muhtasari

Mitandao mingi ya kijamii imeibuka miaka ya hivi karibuni. Kuzuka kwa
mitandao hii kumesababisha mabadiliko makubwa katika lugha, mitindo ya
mawasiliano na mchakato wa mawasiliano. Mawasiliano ya kilugha yamegawika
katika tanzu kuu mbili; yaani mawasiliano ya kimaandishi na yale
yakimazungumzo. Kila utanzu wa mawasiliano ya kilugha una sifa zake bainifu.
Kwa hivyo, lugha ya kimaandishi ni tofauti kisifa na lugha ya kimazungumzo. Hata
hivyo, kuzuka kwa mitandao ya kijamii kumezua lugha ya kidijitali yenye mitindo
ibuka inayodhihirisha sifa mseto za mawasiliano ya kimaandishi ya yale ya
kimazungumzo. Utafiti huu unachunguza lugha ya kidijitali katika Facebook na
kusisitiza kwamba ni lugha ya mazungumzo andishi.

Inahitaji Usajili PDF
Leseni ya Creative Commons

Kazi hii imewekwa chini ya Leseni ya Creative Commons Kutambulisha 4.0 Kimataifa.

Hakimiliki (c) 2024 JARIDA LA CHAUKIDU

Upakuaji

Data ya upakuaji bado haijapatikana.