KISWAHILI KAMA LUGHA RASMI NA LINGUA FRANKA YA AFRIKA MASHARIKI: JE, NI BARAKA AU NI LAANA?
Inahitaji Usajili PDF

Jinsi ya Kunukuu

KISWAHILI KAMA LUGHA RASMI NA LINGUA FRANKA YA AFRIKA MASHARIKI: JE, NI BARAKA AU NI LAANA?. (2024). JARIDA LA CHAUKIDU. https://doi.org/10.0255/ww632a57

##plugins.generic.shariff.share##

Muhtasari

Hadhi ya Kiswahili katika eneo la Afrika Mashariki inatofautiana katika mataifa
tofauti. Nchini Kenya, Kiswahili ni lugha rasmi na pia lugha ya taifa. Nchini
Tanzania, ni lugha ya taifa na pia hutumika katika shughuli nyingi rasmi. Ndiyo
lugha itumiwayo katika kiwango cha elimu ya msingi. Nchini Uganda, Kiswahili
kimeteuliwa kama somo la lazima katika mtaala uliozinduliwa mnamo mwaka
2017. Kilipendekezwa kama lugha rasmi ya pili ya Uganda mnamo mwaka 2005
lakini pendekezo hilo halijapitishwa rasmi. Mnamo mwaka 2017, Bunge la Chini
la Rwanda lilipitisha sheria inayotambua Kiswahili kama lugha rasmi nchini humo.
Makala haya yanatumia nchi hizi nne za Afrika Mashariki kuchunguza maendeleo
ya Kiswahili katika kipindi cha sasa na kuonesha kama maendeleo hayo yana
matokeo chanya au hasi katika mataifa husika na eneo lenyewe. Utafiti utaongozwa
na nadharia iliyoasisiwa na Howard Gile ya Makubaliano ya Mawasiliano (CAT)
lakini ambayo imeendelezwa katika hali nyingi. Yatatumia mihimili yake ya
mwachano na makutano. Makala yanachukulia kwamba maendeleo ya sasa ya
Kiswahili yana manufaa mengi kuliko hasara.

Inahitaji Usajili PDF
Leseni ya Creative Commons

Kazi hii imewekwa chini ya Leseni ya Creative Commons Kutambulisha 4.0 Kimataifa.

Hakimiliki (c) 2024 JARIDA LA CHAUKIDU

Upakuaji

Data ya upakuaji bado haijapatikana.