JARIDA LA CHAUKIDU

Toleo la Sasa

2023
Imechapishwa 1 January 2023
MAKALA YA KONGAMANO LA TATU LA KIMATAIFA LA CHAUKIDU

Tunasikitika kwamba toleo hili la CHAUKIDU halikuweza kutoka kwa wakati uliotarajiwa kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wetu. Tunajua kwamba ni toleo lililosubiriwa na wengi kwa hamu kubwa. Kwa hivyo, tunawaomba wadau wetu wote wakiwemo waandishi wa makala na wasomaji watuwie radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza. Ushirikiano wa wataalamu kutoka maeneo mbalimbali ya dunia ni muhimu kwa taaluma za Kiswahili ambazo zinachangia kwa kiasi kikubwa katika ukuaji wa lugha ya Kiswahili na kuenea kwake duniani. Katika Kongamano lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, mwishoni mwa mwaka wa 2017, wadau kutoka sekta mbalimbali walishiriki na kujadili mchango wa kila tasnia katika kukiendeleza na kukiimarisha Kiswahili. Kongamano lilijadili jinsi kila tasnia ilivyochangia na inavyoendelea kuchangia kwa namna tofautitofauti ukuzaji wa lugha ya Kiswahili na jinsi ambavyo Kiswahili kilichangia na kinaendelea kuchangia kustawisha tasnia husika. Mawasilisho, mazungumzo, na mijadala iliyofanyika iliwasaidia washiriki kuanza kutafakari juu ya uundaji wa dira ya ukuzaji endelevu wa Kiswahili na ustawi endelevu wa jamii katika karne ya 21 kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo. Matokeo ya mijadala yote hiyo ni toleo hili la pili la CHAUKIDU ambalo linajumuisha mawazo ya wadau mbalimbali kupitia mawasilisho yaliyoangazia vipengele mbalimbali kama vile fasihi, isimu, nafasi ya vyombo vya habari katika ukuaji wa Kiswahili na ufunzaji na ujifunzaji wa lugha ya Kiswahili. Katika toleo hili, mada mbalimbali zimeshughulikiwa na waandishi kutokana na tafiti zao za uwandani na mapitio ya maandishi maktabani na kwingineko. Kimsingi basi, kuna makala mengi ambayo yamechapishwa katika toleo hili kuchangia hazina kubwa ya lugha ya Kiswahili. Kazi zilizochapashwa katika toleo hili ni zile zilizoitikia mwito wa mada kuu ya mkusanyiko wa wataalamu mbalimbali kuhusu Dira ya Karne ya 21– Ukuaji wa Kiswahili na Ustawi wa Jamii.

Matangazo

Mwito wa Makala - Jarida la CHAUKIDU

Tunapokea makala kwa ajili ya Toleo la kwanza la Jarida la CHAUKIDU. Tuma makala yako kwa kufuata maelekezo uliyopewa katika fomu hii. Soma zaidi kabla ya kuandaa mswada wako.


Zaidi…

4 March 2024

Makala

Clara Momanyi (Mwandishi)
NAFASI YA KISWAHILI KATIKA UFASIRI WA MIKATABA, SHERIA ZA KITAIFA, NA KIMATAIFA NCHINI KENYA
Inahitaji Usajili PDF (English)
Toboso Mahero Bernard, Mosol Kandagor, Allan Opijah (Mwandishi)
LUGHA YA KIDIJITALI KAMA LUGHA YA KIMAZUNGUMZOANDISHI: MFANO WA MAWASILIANO YA FACEBOOK
Inahitaji Usajili PDF
Gervas A Kawonga (Mwandishi)
KAMISHENI YA KISWAHILI YA AFRIKA MASHARIKI NA HATIMA YA VISWAHILI SANIFU
Inahitaji Usajili PDF (English)
P. I. Iribemwangi Iribemwangi (Mwandishi)
KISWAHILI KAMA LUGHA RASMI NA LINGUA FRANKA YA AFRIKA MASHARIKI: JE, NI BARAKA AU NI LAANA?
Inahitaji Usajili PDF
Leah Y. Kiloba, Getruda E Shima (Mwandishi)
JAZANDA YA MAJINA YA MAONESHO KATIKA TAMTHILIA ZA KISWAHILI: MIFANO YA TAMTHILIYA ZA NGOSWE PENZI KITOVU CHA UZEMBE NA CHANZO NI WEWE
Inahitaji Usajili PDF
Hadija Jilala (Mwandishi)
TAFSIRI BINAFSI KATIKA NADHARIA YA TAFSIRI: UTHABITI, CHANGAMOTO NA MAPENDEKEZO
Inahitaji Usajili PDF
Sarah Ndanu M. Ngesu, Leonard Muaka (Mwandishi)
DHIMA NA CHANGAMOTO ZA MATUMIZI YA TAFSIRI KATIKA UFUNDISHAJI WA KISWAHILI NCHINI UGANDA
Inahitaji Usajili PDF
Fokas Nchimbi (Mwandishi)
MATUMIZI YA FASIHI SIMULIZI KATIKA KAMPENI ZA UCHAGUZI TANZANIA: TATHMINI YA DHIMA YA NYIMBO
Rose Jackson Mbijima (Mwandishi)
MATUMIZI YA LUGHA KATIKA RIWAYA YA KWANZA YA KISWAHILI YA UHURU WA WATUMWA NA RIWAYA YA KWANZA YA KISWAHILI YA MAJARIBIO YA NAGONA
Inahitaji Usajili PDF
Anne Jebet (Mwandishi)
MITAZAMO YA LUGHA NA ELIMU KATIKA JAMII ZA AFRIKA MASHARIKI
Inahitaji Usajili PDF
Issaya Lupogo (Mwandishi)
MZUNGUKO WA UKANUSHI WA JESPERSEN KATIKA LUGHA YA KISWAHILI
Inahitaji Usajili PDF
Justus Kyalo Muusya (Mwandishi)
MWINGILIANOMATINI KATIKA USAWIRI WA MWANAMKE KATI YA TAMTHILIA ZA KILIO CHA HAKI YA A. MAZRUI NA KIGOGO YA P. KEA
Inahitaji Usajili PDF
Felix Sosoo (Mwandishi)
RUWAZA YA SHUJAA YA CAMPBEL: TOFAUTI ZINAZOONESHWA NA NGANO TEULE ZA KIEWE KUTOKA GHANA
Inahitaji Usajili PDF
Ahmad Sovu (Mwandishi)
MOFIMU SABABISHI -Z- KATIKA KITENZI CHA KISWAHILI
Inahitaji Usajili PDF
James Marwa Mwita (Mwandishi)
TATHMINI YA MCHANGO WA VYOMBO VYA HABARI VYA KICHINA KATIKA KUKUZA NA KUENEZA KISWAHILI
Inahitaji Usajili PDF
Mulei Martin (Mwandishi)
UCHANGANUZI WA MWINGILIANO WA MANENO KATIKA MAZUNGUMZO KWA KISWAHILI MIONGONI MWA WANAFUNZI WA SHULE YA UPILI UGANDA
Inahitaji Usajili PDF
Naomi Musembi (Mwandishi)
UNAFIKI WA VIONGOZI WA KISIASA KAMA MKAKATI WA KUWAWEKA MAMLAKANI: MFANO KUTOKA RIWAYA ZA KATAMA MKANGI: MAFUTA NA WALENISI
Inahitaji Usajili PDF
Tazama Matoleo Yote

Jarida la CHAUKIDU ni jarida la kitaaluma linalochapishwa na Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani (CHAUKIDU) na kusambazwa katika nakala ngumu na nakala-pepe. Jarida hili ni la kitaaluma na huchapishwa mara moja kwa mwaka katika lugha ya Kiswahili. Jarida hili huchapisha makala juu ya taaluma za Kiswahili ambazo hazijachapishwa kwingine wala hazijawasilishwa kuchapishwa katika jarida jingine au machapisho mengine.  Makala za jarida hili zitatathminiwa  kwa kufichisha (tathmini-fiche) ambapo watakaotathmini hawatamjua mwandishi wa makala. Jarida hili linapatikana katika tovuti ya chama.