Tunapokea makala kwa ajili ya Toleo la kwanza la Jarida la CHAUKIDU. Tuma makala yako kwa kufuata maelekezo uliyopewa katika fomu hii.
Mwongozo kwa WaandishiJarida hili litachapisha makala za kitaalamu za fasihi, isimu, na utamaduni wa Kiswahili. Taaluma mbalimbali katika tanzu za kimapokeo na pia tanzu mpya zinazoibuka hasa kutokana na maendeleo ya teknolojia.
- Ufundishaji wa lugha
- Isimu: km fonetiki, fonolojia, mofolojia, semantiki, isimu linganishi, isimu jamii, nk
- Fasihi: fasihi simulizi, fasihi andishi,
- Ulinganifu wa Kiswahili na lugha nyingine za Afrika.
- Utamaduni wa Waswahili na wazungumzaji wa Kiswahili
- Sera na matumizi ya lugha
- Maendeleo ya Kiteknolojia
Waandishi wanakaribishwa kuwasilisha makala katika jarida hili. Miswada yote itachunguzwa na mhariri ili kujua kama inakidhi malengo na wigo wa jarida hili. Ile itakayoonekana kuwa inafaa itatumwa kwa watathmini-rika kabla ya kuamuliwa ikiwa itakubaliwa au kukataliwa.
Kabla ya kuwasilisha miswada yao, waandishi wanawajibika kupata ruhusa ya kuchapisha nyenzo zote zilizomo kwenye miswada, kama picha, nyaraka na seti za data. Waandishi wote waliotambuliwa kwenye miswada wanapaswa kukubali kutambuliwa kama wandishi. Kulingana na mahitaji ya kisheria ya nchi ya utafiti, utafiti unapaswa kupitishwa na kamati sahihi ya maadili ya kitafiti ikiwa inahitajika hivyo.
Mhariri anaweza kukataa mswada ikiwa haukidhi viwango vya chini vya ubora. Kabla ya kuwasilisha mswada wako, tafadhali hakikisha muundo wa utafiti na hoja ya utafiti vimeandikwa na kuelezewa kwa usahihi. Anuani ya mswada inapaswa kuwa fupi na muhtasari unapaswa kuwa mzuri. Hii itaongeza uwezekano wa watathmini kukubali kufanya tathmini ya mswada wako. Ukiridhika kwamba mswada wako unakidhi kiwango hicho, tafadhali fuata orodha-hakiki iliyo hapa chini ili kuandaa mswada wako.
Maelekezo Muhimu kwa Uaandaaji wa Mswada
- Miswada iandikwe katika mfumo wa MS Word na kuwasilishwa kwa wahariri kwa kutumia mfumo maalumu upatikanao katika tovuti yetu. Tuma Mswada kwa Kubofya Hapa.
- Mswada mzima uandikwe kwa hati ya Garamond.
- Isipokuwa tu maeneo machache ambayo utapewa maelekezo mahususi, aya zote ziandikwe kwa ukubwa wa pt. 11.
- Pambizo ziwe na pt. 1 kwa upande wa juu na upande wa chini. Pambizo ziwe na pt. 1.5 kwa upande wa kushoto na kulia.
- Ili kusaidia tathmini-fichishi, wasilisha mswada wako bila kuweka jina lako, wala vidokezo vyovyote vya majina ya waandishi, taasisi wanakofanyia kazi, anuani-pepe zao, na nambari za ORCID kama wanazo. Makala ambazo hazitazingatia maelekezo haya, zitakataliwa na hazitafanyiwa tahakiki.
- Taarifa kuhusu mwandishi/waandishi wa mswada, lazima zijazwe katika fomu maalumu ya kupokelea makala.
- Mswada ifanyiwe uhariri wa kina kabla ya kuwasilishwa katika jarida.
- Urefu wa mswada uwe ni maneno kati ya 3000 na 7000.
- Anuani ya mswada na vichwa vya sehemu zote za mswada viandikwe kama vinavyoonekana katika Sampuli ya Mswada.
- Ikisiri: Ikisiri isizidi maneno 250. Ikisiri isiwe na tanbihi za chini ya ukurasa wala isiwe na marejeleo.
- Chini ya ikisiri paandikwe maneno muhimu ya makala/mswada.
- Marejeleo: Tumia mtindo wa APA toleo la 7. Unaweza kupata maelezo kuhusu APA kwa kutumia kiungo Hiki Hapa.
- Usitumie tanbihi isipokuwa tu pale ambapo kuna ulazima huo. Tanbihi, ikiwa itatumiwa iwe kama ifuatavyo: Tumia fonti ya 10 pt na tanbihi zitambulishwe kwa tarakimu 1, 2, 3, nk.
- Nukuu: Data na maneno kutoka lugha nyingine yaandikwe kwa italiki. Tafsiri za maneno ya kigeni ziwe katika alama za nukuu moja (`) na alama za nukuu mbili (“) zitatumika kuonesha nukuu za aina nyingine.
- Fungua hapa kupata Sampuli ya mswada wa awali
Kwa maelezo zaidi, soma ukurasa wetu wa Miswada.