JAZANDA YA MAJINA YA MAONESHO KATIKA TAMTHILIA ZA KISWAHILI
Requires Subscription PDF (Swahili)

How to Cite

JAZANDA YA MAJINA YA MAONESHO KATIKA TAMTHILIA ZA KISWAHILI: MIFANO YA TAMTHILIYA ZA NGOSWE PENZI KITOVU CHA UZEMBE NA CHANZO NI WEWE. (2024). JARIDA LA CHAUKIDU. https://doi.org/10.0255/2e8h5b30

Share

Abstract

Makala haya yanahusu jazanda ya majina ya maonesho katika tamthiliya za
Kiswahili: huku mifano ikitolewa kutoka tamthilia za Ngoswe Penzi Kitovu cha
Uzembe ya E. Semzaba na Chanzo ni Wewe ya W. Himu. Makala yanachambua
jinsi jazanda zilizotumika kubuni majina ya maonesho zinavyosaidia kudokeza
mawazo ya msingi katika onesho husika. Mjadala unajikita kuonesha namna
watunzi hao walivyoepuka majina zoefu ya maonesho ambayo pengine ni majina ya
kimapokeo. Tamthiliya nyingi hutumia majina kama vile onyesho, kitendo, sehemu
n.k. Watunzi hawa wamekuwa wabunifu kwa kukiuka kaida fulani zilizozoeleka
na kutoa majina yenye kutafakarisha zaidi. Mwisho, makala yanaonesha jinsi
jazanda za majina ya maonesho katika tamthiliya teule zinavyoakisi migongano ya
wahusika ndani ya maonesho ya tamthilia hizo. Uakisi huo unajibainisha katika
mfuatano, muendelezano na mkamilishano wa matukio, vitendo na maonyesho ndani
ya tamthiliya hizo. Nadharia ya Usasa ndiyo mwongozo wa ufafanuzi wa makala
haya. Nadharia hii hutumiwa kuzielezea au kuzitambulisha sifa mpya za dhamira,
tanzu, dhana na mitindo ya kifasihi inayojitenga na misingi na jadi ya sanaa na
utamaduni wa Kimagharibi au uliokuwapo.

Requires Subscription PDF (Swahili)
Creative Commons License

This work is licensed under a Creative Commons Attribution 4.0 International License.

Copyright (c) 2024 JARIDA LA CHAUKIDU

Downloads

Download data is not yet available.