TAFSIRI BINAFSI KATIKA NADHARIA YA TAFSIRI: UTHABITI, CHANGAMOTO NA MAPENDEKEZO
Requires Subscription PDF (Swahili)

How to Cite

TAFSIRI BINAFSI KATIKA NADHARIA YA TAFSIRI: UTHABITI, CHANGAMOTO NA MAPENDEKEZO. (2024). JARIDA LA CHAUKIDU. https://doi.org/10.0255/0nqjfk41

Share

Abstract

Nadharia ya tafsiri ni taaluma kongwe ulimwenguni ambayo imesaidia kukuza
uchumi na maendeleo ya jamii kwa kurahisisha mawasiliano na kuunganisha
ulimwengu. Tunapozungumzia tafsiri binafsi ni ile tafsiri inayofanywa na mwandishi
wa matini chanzi kwa kuhawilisha mawazo ama ujumbe wa lugha chanzi kwenda
lugha lengwa ambayo ni tofauti na ile aliyoitumia kuandikia matini ya awali. Swali
la kujiuliza katika mchakato wa kutafsiri matini binafsi ni: je, mfasiri anatafsiri
ama anahamisha mawazo yake aliyoyaandika kwa kutumia lugha chanzi na
kuyaandika kwa kutumia lugha nyingine (lugha lengwa)? Je, ni mbinu zipi
zinazotumika katika kutafsiri matini binafsi? Je, mfasiri binafsi hukumbana na
changamoto zipi anapotafsiri matini yake? Kwa hiyo, makala haya inachunguza
tafsiri binafsi katika nadharia ya tafsiri ili kubaini mbinu zinazotumika katika
tafsiri binafsi, kubainisha changamoto za tafsiri binafsi na kutoa mapendekezo
kuhusu tafsiri binafsi katika nadharia ya tafsiri. Ili kufikia malengo hayo, makala
haya yametumia mifano ya matini mbili za fasihi, yaani riwaya ya Bwana
Myombekere na Bibi Bugonoka Ntutalanalwo na Bulihwali (1980) iliyoandikwa na
kutafsiriwa na Anicent Kitereza na tamthiliya ya Mtawa Mweusi (1970) ambayo ni
tafsiri ya The Black Hermit (1968) tamthiliya iliyoandikwa na Ngugi wa Thiong’o
na kisha kuitafsiri kwa lugha ya Kiswahili. Data za makala haya zilikusanywa
kwa kutumia mbinu tatu, yaani mbinu ya usomaji wa machapisho, dodoso na usaili.
Kwa kutumia Nadharia ya Ulinganifu, makala haya yanajadili kuwa tafsiri binafsi
ni ile ambayo huzingatia nadharia na vitendo, kwa hiyo, mfasiri hukumbana na
changamoto za kiisimu, kiutamaduni na kimaana katika mchakato wa tafsiri kama
ilivyo katika tafsiri inayofanywa na mtu mwingine. Kwa hiyo, ujuzi wa lugha,
utamaduni na nadharia za tafsiri ni mambo ya msingi katika kufanikisha
mawasiliano ya kazi ya tafsiri bila kujali ni tafsiri binafsi au tafsiri inayofanywa na
mtu mwingine.

Requires Subscription PDF (Swahili)
Creative Commons License

This work is licensed under a Creative Commons Attribution 4.0 International License.

Copyright (c) 2024 JARIDA LA CHAUKIDU

Downloads

Download data is not yet available.