MITAZAMO YA LUGHA NA ELIMU KATIKA JAMII ZA AFRIKA MASHARIKI
Requires Subscription PDF (Swahili)

How to Cite

MITAZAMO YA LUGHA NA ELIMU KATIKA JAMII ZA AFRIKA MASHARIKI. (2024). JARIDA LA CHAUKIDU. https://doi.org/10.0255/nhn3m586

Share

Abstract

Nchi nyingi za Afrika Mashariki na barani Afrika zimejaliwa kuwa na idadi
kubwa za lugha. Ni jambo la kawaida kukuta lugha zaidi ya mia moja
zinazozungumzwa katika nchi moja pekee. Hali hii imeleta utata na hata
kusababisha baadhi ya lugha kukosa wasemaji (Brock-Utne na wenzie, 2010).
Kiswahili, lugha ya taifa nchini Kenya na Tanzania ni mojawapo ya lugha
zinazokabiliwa na utata mkubwa hasa kuhusu matumizi yake kama lugha ya
kufundishia au kufundishwa katika mifumo ya elimu. Huku wadau wengi wa lugha
wakihimiza matumizi ya lugha itakayomwezesha mwanafunzi kujifunza na
kuyaelewa mazingira yake, bado kuna athari kubwa katika kukabiliana na
ulimwengu wa utandawazi. Makala haya yanakusudia kuchambua kwa undani
zaidi mitazamo ya lugha katika Afrika ya Mashariki (nchi za Kenya na Tanzania)
na kulinganua mitazamo ya lugha na umuhimu wake katika kupiga vita dhidi ya
kasumba ya kikoloni na utumwa wa Kiingereza. Ingawa tafiti nyingi zimeeleza zaidi
kuhusu sera za lugha katika nchi hizi, makala haya yanatoa hoja kuwa mitazamo
ya lugha imeathiriwa sana na sera hizo za lugha na zaidi pia mambo mengine kama
ubeberu wa kiisimu na utandawazi. Hivyo basi, tutachunguza jinsi makala na tafiti
mbalimbali katika nchi hizi mbili, zilivyozungumzia masuala haya tangu wakati wa
ukoloni hadi miaka ya karibuni na iwapo kumekuwa na mabadiliko yoyote.

Requires Subscription PDF (Swahili)
Creative Commons License

This work is licensed under a Creative Commons Attribution 4.0 International License.

Copyright (c) 2024 JARIDA LA CHAUKIDU

Downloads

Download data is not yet available.