KAMISHENI YA KISWAHILI YA AFRIKA MASHARIKI NA HATIMA YA VISWAHILI SANIFU
Requires Subscription PDF

How to Cite

KAMISHENI YA KISWAHILI YA AFRIKA MASHARIKI NA HATIMA YA VISWAHILI SANIFU. (2024). JARIDA LA CHAUKIDU. https://doi.org/10.0255/1bhn3917

Share

Abstract

Makala haya yanahusu nafasi ya Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki
(KAKAMA) ikiwa ni tumaini jipya katika kudhibiti Viswahili sanifu katika nchi
za Afrika Mashariki. Makala haya ni matokeo ya utafiti wa maktabani uliohakiki
maandiko mbalimbali. Hoja kuu ya makala haya ni kwamba wakati wa ukoloni
kulikuwa na Kiswahili sanifu cha Afrika Mashariki ambacho hakipo katika
Afrika Mashariki huru. Hii ni kwa sababu, baada ya uhuru, Kamati ya Lugha
(Kiswahili) ya Afrika Mashariki ilisambaratika na huo ukawa mwanzo wa
kuibuka na kukua kwa Viswahili sanifu vya kimaeneo. Kuundwa kwa BAKITA
Tanzania Bara na BAKIZA kwa upande wa Zanzibar kuliimarisha launi za
Kiswahili. Pia, kutungwa kwa kamusi za KKS, KKF na KTK kwa Tanzania,
Zanzibar na Kenya mtawalia ni ushahidi wa kuimarika kwa Viswahili sanifu vya
kimaeneo. Vichocheo vya kuinukia kwa Viswahili hivyo vinaweza kuwa vingi lakini
mawanda ya kisiasa kama kipengele muhimu cha ikolojia ya lugha yana nafasi ya
juu zaidi kuliko sababu kuntu za kitaaluma. Hitimisho la makala haya ni kwamba
inafaa kuwe na usanifishaji mpya na endelevu wa Kiswahili ili kurejesha umoja wa
lugha wa Afrika Mashariki uliokuwapo wakati wa ukoloni. Wito wa makala haya
ni kwamba KAKAMA inapaswa kuchukua hatua zinazostahiki kusitisha
ongezeko la Viswahili sanifu kwa madai ya uhuru wa jamii kutumia lugha itakavyo.
Muhuri wa ithibati lazima urejeshwe kwa KAKAMA ili kuhakikisha kwamba
msamiati, miundo na matumizi ya Kiswahili sanifu kwa jumla yanasawazishwa.
Matumizi rasmi ya lugha kama vile katika elimu na utawala yanapaswa kuwa yale
yaliyokubaliwa na watumiaji kwa vigezo vya pamoja.

Requires Subscription PDF
Creative Commons License

This work is licensed under a Creative Commons Attribution 4.0 International License.

Copyright (c) 2024 JARIDA LA CHAUKIDU

Downloads

Download data is not yet available.