MOFIMU SABABISHI -Z- KATIKA KITENZI CHA KISWAHILI
Requires Subscription PDF (Swahili)

How to Cite

MOFIMU SABABISHI -Z- KATIKA KITENZI CHA KISWAHILI. (2024). JARIDA LA CHAUKIDU. https://doi.org/10.0255/9bneqe62

Share

Abstract

Mojawapo ya michakato ya uambishaji ni unyambuaji wa kitenzi. Kwa kawaida,
unyambuaji huo wa kitenzi huwa haufanyiki kihobelahobela bali kuna mofimu
mbalimbali ambazo huambikwa na kuleta unyumbuaji wa kitenzi hicho.
Unyambuaji wa mofimu hizo hutawaliwa na kanuni mbalimbali zinazoonesha kauli
za kutenda, kutendea, kutendwa, kutendesha n.k. Katika lugha ya Kiswahili,
kanuni za unyambuaji zimeundwa na wanaisimu mbalimbali kama vile Ashton
(1944), Streere (1950), Polome (1967), Broomfield (1975) na Kapinga (1983)
(Kiango 2008). Miongoni mwa kanuni hizo ni kanuni ya utenda, utendwa, utendeka,
usababishi, utendana na kadhalika. Kila kanuni ina kanuni nyingine ndogondogo
ndani mwake, hata hivyo, makala haya yameangazia kanuni ya usababishi.
Japokuwa kuna kanuni nyingi za usababishi, makala haya yamejikita katika
kanuni ya usababishi ya -z- ambayo inafafanuliwa kuwa katika mzizi wa kitenzi
kinachoishia na mkururo wa irabu, kwa mfano, kitenzi pa-a katika hali ya
usababishi huwa pa-z-a, li-a huwa li-z-a n.k. Kwa ujumla, makala haya
yanajaribu kuchunguza iwapo kanuni inafuatwa na vitenzi vyote vya Kiswahili sanifu
na fasaha au la. Matokeo ya uchunguzi huu yanaonesha kuwa baadhi ya vitenzi vya
Kiswahili sanifu havifuati kanuni hii katika kupata hali ya usababishi. Kwa mfano,
vitenzi ondoa huwa ondo-sh-a, roa huwa ro-vy-a n.k. Makala yanapendekeza
kuwa kanuni mbalimbali zilizoundwa na wataalamu wa zamani zichunguzwe tena
ili kuziweka sawa na kuondosha utata na vighairi vinavyojitokeza katika kanuni
hizo.

Requires Subscription PDF (Swahili)
Creative Commons License

This work is licensed under a Creative Commons Attribution 4.0 International License.

Copyright (c) 2024 JARIDA LA CHAUKIDU

Downloads

Download data is not yet available.