Abstract
Mitandao mingi ya kijamii imeibuka miaka ya hivi karibuni. Kuzuka kwa
mitandao hii kumesababisha mabadiliko makubwa katika lugha, mitindo ya
mawasiliano na mchakato wa mawasiliano. Mawasiliano ya kilugha yamegawika
katika tanzu kuu mbili; yaani mawasiliano ya kimaandishi na yale
yakimazungumzo. Kila utanzu wa mawasiliano ya kilugha una sifa zake bainifu.
Kwa hivyo, lugha ya kimaandishi ni tofauti kisifa na lugha ya kimazungumzo. Hata
hivyo, kuzuka kwa mitandao ya kijamii kumezua lugha ya kidijitali yenye mitindo
ibuka inayodhihirisha sifa mseto za mawasiliano ya kimaandishi ya yale ya
kimazungumzo. Utafiti huu unachunguza lugha ya kidijitali katika Facebook na
kusisitiza kwamba ni lugha ya mazungumzo andishi.
This work is licensed under a Creative Commons Attribution 4.0 International License.
Copyright (c) 2024 JARIDA LA CHAUKIDU